Stori za Mastaa

“SIJAWAHI KUVUTIWA KIMAPENZI NA WANAUME WENYE SURA NZURI” -IRENE UWOYA

Feb 08, 2017 adam

Hujiamini kutupa karata yako kwa muigizaji mrembo Irene Uwoya sababu unahisi huna sura nzuri na ya kuvutia? Basi unaichezea bahati yako sababu unaweza kuwa na nafasi kubwa zaidi.

Kwa mujibu wa Irene, wanaume wenye sura mbaya ndio ambao huamsha zaidi hisia zake za kimapenzi! Strange, lakini ndio ukweli wake. Muigizaji huyo ambaye ameandaa event maalum kwaajili ya Valentine’s Day aliyoipa jina, ‘Irene Uwoya Valentine’s Special Night, ameahidi kueleza baadhi ya mambo ambayo watu hawafahamu kuhusu yeye katika sekta ya malavidavi.

“Kitu ambacho hamkijui kuhusu mimi ni kuwa sijawahi kuvutiwa na wanaume wenye mionekano mizuri, sielewi ni kwanini lakini wanaume wenye sura mbaya huwa wanaamsha hisia zangu za KIMAPENZI,” ameandika Uwoya.

Wanaume wenye sura nzuri, poleni!

Sambaza Makala hiiShare on FacebookTweet about this on TwitterShare on LinkedInShare on Google+

Comments

comments