Stori za Mastaa

LEBO YA UNIVERSAL MUSIC GROUP YATANGAZA RASMI KUMSAJILI DIAMOND PLATNUMZ

Feb 03, 2017 adam

Hatimaye record label kubwa duniani, Universal Music Group (UMG), imemtangaza rasmi kumsainisha Diamond Platnumz.

Anakuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kusainishwa kwenye label hiyo.

Wimbo wake, Marry You akiwa na Ne-Yo ni wa kwanza kutoka chini ya mwamvuli wa Universal Music.

“Yeye ni nyota, ana kipaji na nguvu na ubunifu na yupo kwenye anga moja na wanamuziki wa kimataifa ambao nafanya nao kazi” anasema Mkurugenzi Mtendaji wa label hiyo Afrika, Sipho Diamini.

“Yupo makini na anapenda mafanikio. Anapenda nchi yake, watu wake, lugha yake na utamaduni wake na nimependa hilo. Ana kiwango cha hali ya juu sana katika kutumbuiza jukwaani na ana uhalisia wa kiafrika na hilo litawagusa sana watu wengi ulimwenguni. Wasanii kama yeye ni sababu ya sisi kufanya tunachokifanya”

Sambaza Makala hiiShare on FacebookTweet about this on TwitterShare on LinkedInShare on Google+

Comments

comments