Burudani Stori za Mastaa

LADY JAYDEE ABADILISHA UKUMBI KWA AJILI YA UZINDUZI WA ALBAMU YAKE MPYA LEO

Mar 31, 2017 adam

Lady Jaydee leo atafanya uzinduzi wa album yake mpya na ya saba, Woman.

Ametangaza kubadilisha ukumbi wa awali na sasa utafanyika King Solomon Hall.

“Naomba kuwafahamisha mabadiliko ya Venue Ijumaa Woman Album Launch Itafanyika ukumbi wa King Solomon Hall , karibu na Best Bite (Ada Estate- Kinondoni) Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza,” ameandika Jide kwenye Instagram.

Album hiyo itakuwa na nyimbo kama Kamoba alioshirikiana na Hamoba wa Zambia, Together Remix akiwa na Spicy, Rosella akiwa na H_Art the Band, Unanichanganya akiwa na Naava wa Uganda na zingine.

Sambaza Makala hiiShare on FacebookTweet about this on TwitterShare on LinkedInShare on Google+

Comments

comments