Stori za Mastaa

“KATI YA BARAKA THE PRINCE NA LORD EYEZ SIONI WA KUMUONGOZA MWENZIE”, NAY WA MITEGO ANG’AKA

Feb 08, 2017 adam

Msanii wa muziki wa hip hop Nay wa Mitego amedai kitendo cha Baraka The Prince kumsaini aliyekwa member wa kundi la Weusi, Lord Eyez itakuwa ni safari ya kipofu na kiziwi.

Miezi michache iliyopita Baraka Da Prince alitangaza kutaka kumsaini Lord Eyez huku uongozi wa Weusi ukidai hauna taarifa hizo na wao wanazisikia tetesi hizo kupitia mitandao ya kijamii.

Akizungumzia suala hilo katika 255 ya XXL ya Clouds FM, rapper Nay wa Mitego amedai kati ya Barakah na Lord Eyez haoni wa kumuongoza mwenzake.

“Hiyo ni safari ya kipofu na kiziwi, naweza kusema hivyo. Kiukweli haimake sense, kwasababu mtu ambaye anataka kuongozwa na yeye akamuongoza mwenziye ndio maana ya mfano wangu. Kibaya zaidi Lord Eyez ni mkubwa zaidi ya Baraka. Sawa kuna watu ambao wanasimamiwa na watu wadogo lakini ukiangalia pale alipo msanii kama Baraka anahitaji msaada zaidi.” alisema Nay wa Mitego.

Suala hilo limeleta mjadala katika mitandao ya kijamii huku wengi wakiendelea kusubiri kuona itakuwaje.

Sambaza Makala hiiShare on FacebookTweet about this on TwitterShare on LinkedInShare on Google+

Comments

comments