Stori za Mastaa

HUYU NDIYE YULE SHEMEJI MCHINA AMBAYE OMMY DIMPOZ ALITUAHIDI?

Feb 08, 2017 adam

Msanii Ommy Dimpoz ambaye anafanya vyema na wimbo wake ‘Kajiandae’ wiki kadhaa zilizopita alifunguka na kusema ikifika wakati ataweka wazi suala la mahusiano yake kwa jamii, na kumuweka wazi mchumba wake ili watu wajue.

Ommy Dimpoz alisema hayo kwenye kipindi cha eNewz cha EATV wiki kadhaa zilizopita, Ommy alifunguka na kuthibitisha kuwa kwa sasa yupo kwenye mahusiano na raia wa China., ambaye watu wengi hawamjui.

Juzi Ommy Dimpoz ametupia Instagram picha ya pamoja akiwa na binti huyo mwenye asili ya China kisha akaweka ’emoji’ yenye ishara ya love, akiashiria ‘Mapenzi bampa 2 bampa’.

Ingawa Ommy Dimpoz hakutaka kufungua mjadala kwenye picha ile kwa kuamua kufunga uwanja wa comment ili watu wasiweze kuzungumza wala kujadili katika picha hiyo. Lakini ukweli ni kwamba picha ile inazungumza mambo mengi kwa kila anayeiangalia.

 

Sambaza Makala hiiShare on FacebookTweet about this on TwitterShare on LinkedInShare on Google+

Comments

comments